Na Lydia Lugakila-Misalaba Media, MbeyaMkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, ameungana na viongozi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Kampasi ya Mbeya, katika ziara maalum ya kugusa maisha ya watoto wenye mahitaji maalum na yatima. Ziara hiyo ilihusisha utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa chuo hicho.Katika ziara hiyo, ujumbe huo ulitembelea Kituo cha Bi. Aisha Foundation kilichopo Soweto pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Iwambi. Walipata fursa ya kukutana na watoto hao, kusikiliza changamoto zao, na kushiriki nao kwa karibu katika mazingira ya upendo na faraja.Mhe. Itunda alikabidhi vyakula mbalimbali vilivyotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma, akieleza kuwa hatua hiyo inaakisi dhamira ya dhati ya taasisi hiyo katika kushiriki maendeleo ya jamii na kusaidia makundi yenye uhitaji maalum.Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuweka mkazo katika ustawi wa jamii, hususan kwa makundi yenye uhitaji maalum.Kwa upande wao, viongozi wa vituo hivyo walishukuru kwa msaada huo, wakibainisha kuwa utachangia kuboresha maisha ya watoto wanaolelewa katika vituo hivyo. Pia walitoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia makundi hayo yenye uhitaji.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment