" MWANAMKE AUAWA KATIKA MAZINGIRA YA UTATA SHINYANGA

MWANAMKE AUAWA KATIKA MAZINGIRA YA UTATA SHINYANGA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hollo Ruchanganya, mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa Kijiji cha Bunambiyu Wilaya ya Kishapu, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi, amesema kuwa tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina, ambapo bado baadhi ya watu wanaendelea kujihusisha na vitendo hivyo hatarishi.

Amesema tukio hilo lilianzia nyumbani kwa marehemu baada ya mgeni asiyejulikana kufika majira ya usiku wakati familia ikiandaa chakula cha jioni, na kujitambulisha kuwa anatoka Kijiji cha Sanga, Mwamashimba Wilaya ya Kwimba.

Kwa mujibu wa Kamanda Magomi, mgeni huyo aliomba apelekwe kwa mganga wa jadi anayejulikana kwa jina la Ng’wana Masanja, ambaye ni ndugu wa marehemu, na baada ya mazungumzo, marehemu aliondoka naye kwa lengo la kumpeleka.

“Hata hivyo, tangu aondoke na mgeni huyo hakurejea nyumbani, na baadaye mwili wake ulikutwa majira ya asubuhi na ndugu yake aliyekuwa akielekea shambani,” amesema Magomi.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mtu aliyekuwa na marehemu kabla ya kifo chake ili aweze kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria, huku likisisitiza kuwa halitavumilia vitendo vya mauaji vinavyochochewa na imani potofu za kishirikina.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bunambiyu, Boniphace Zengo, amesema alipokea taarifa za tukio hilo majira ya saa moja asubuhi na kufika eneo la tukio, ambapo alishirikiana na wananchi pamoja na familia ya marehemu kupata taarifa za awali.

Amesema familia ilieleza kuwa mgeni huyo alifika majira ya saa tatu usiku akitafuta waganga wa mapacha na kuelekezwa kwa mtu anayejulikana kama Ng’wana Masanja, ndipo marehemu alipoamua kuongozana naye baada ya kumaliza kula chakula.

Hata hivyo, marehemu hakurejea nyumbani na kwamba alikutwa akiwa ameuawa kisha mwili wake kutupwa katika shamba la mahindi jirani na makazi yake katika kijiji cha Bunambiyu, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post