Na, Egidia Vedasto,Misalaba Media, Arusha.Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, amepongeza juhudi za wanasheria kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao na kuahidi kushughulikia changamoto zote ili kuweka mazingira bora zaidi mahali pa kazi.Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanyika Jijini Arusha, amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji, kuzingatia maadili ya kazi, na kuepuka rushwa.Aidha, amewataka watumishi pamoja na wadau wa sekta ya sheria kuisoma na kuielewa vyema Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, akibainisha kuwa ofisi yake ina jukumu kubwa katika kuhakikisha Dira hiyo inatekelezwa kikamilifu kwa manufaa ya taifa."Utekelezaji mzuri wa majukumu na usimamizi imara wa sheria utasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo ya nchi".Pia amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia malengo na vipaumbele vya taasisi.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TUGHE katika ofisi hiyo, Rashid Kigalu amesema watumishi wanathamini fursa wanazopewa, ikiwemo mafunzo ya afya na mafunzo ya ndani kuhusu uwajibikaji, ambayo yameongeza ufanisi kazini na kuchangia ongezeko la bajeti ya ofisi.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment