Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi, Iddi
Hassan Kimanta, amekamilisha ziara ya siku saba katika kata zote 27 za Wilaya
ya Mpanda iliyofanyika kuanzia Aprili 9 hadi 15, 2026, akikutana na wanachama
na viongozi wa ngazi mbalimbali.
Katika ziara hiyo, Kimanta alilenga kuwasalimia
wanachama, kuwashukuru kwa ushindi mkubwa wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na
kuhimiza mshikamano katika kukijenga chama. Alisema mafanikio yaliyopatikana
yanatokana na umoja, juhudi na ushirikiano wa wanachama katika ngazi zote.
Aidha, aliwataka wanachama kuendelea kuimarisha uhai
wa chama kwa kulipa ada na kusajili wanachama wapya, huku akizihimiza jumuiya
zake za Umoja wa Vijana wa CCM, Umoja wa Wanawake wa Tanzania na wazazi
kuongeza kasi ya uhamasishaji katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Kimanta aliahidi kutoa vyeti
vya shukrani kwa kila kata kama ishara ya kuthamini mchango wa wanachama katika
kuimarisha chama na kuleta ushindi. Pia aliwataka wanachama kuendeleza upendo,
amani na mshikamano bila kujali nafasi au cheo.
Ziara hiyo pia ilitumika kuwapongeza madiwani, wabunge
na viongozi mbalimbali wa mkoa huo kwa ushirikiano wao, huku akitolea mfano
mafanikio ya kupatikana kwa mbunge wa tatu wa viti maalum mkoani Katavi.
Akizungumza na wanachama katika kata mbalimbali,
Kimanta alisisitiza umuhimu wa kujenga mahusiano mazuri ndani ya chama,
kusikiliza na kutatua kero za wanachama pamoja na kusonga mbele katika
utekelezaji wa majukumu ya chama bila kukwama.
Katika hitimisho la ziara hiyo, alielekeza viongozi wa
ngazi za matawi, mashina, kata na wilaya kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa
wanachama, kufanya vikao vya mara kwa mara, kuandika kumbukumbu sahihi, kubuni
miradi ya maendeleo na kuimarisha nidhamu pamoja na mawasiliano ndani ya chama.
Ziara hiyo ilihusisha kata zote 27 za Wilaya ya Mpanda, zikiwemo Kashaulili, Majengo, Misunkumilo, Kakese, Ibindi, Katumba, Mtapenda na Ugalla, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha chama katika ngazi ya msingi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
























































































































































Post a Comment