Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Tanzania ipo imara na inaendelea kupiga hatua kubwa za kimaendeleo wakati huu nchi ikiazimia kutimiza miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza jana wakati akifungua kongamano la miaka 62 ya Muungano lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) katika Chuo cha Vijana Tunguu, Kusini Unguja, Rais Samia amebainisha kuwa nchi imepata mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kisiasa, na kiteknolojia kutokana na misingi ya amani na utulivu iliyowekwa na waasisi wa taifa hili.
Katika hotuba yake, Rais Samia ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Julius Nyerere, na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, kwa uamuzi wao wa kishujaa na wenye maono ya mbali wa kuunganisha mataifa haya mawili.
Amesisitiza kuwa Muungano huu si wa serikali pekee bali ni wa wananchi, na ametoa rai kwa kila mtanzania kuendelea kuulinda na kuutukuza kama urithi adhimu uliolenga kujenga taifa lenye nguvu, mshikamano, na ustawi wa pamoja kwa vizazi vyote.
Rais ametoa onyo kali kwa vijana dhidi ya matumizi ya misamiati na teminolojia mpya zinazochochea ubaguzi na utengano miongoni mwao, akisema kuwa mienendo hiyo inahatarisha mshikamano wa kitaifa.
Amewaalika vijana kutafakari kwa kina umuhimu wa kushikamana kwani kufanya hivyo kunawanyima maadui nafasi ya kuivuruga nchi, huku akibainisha kuwa kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022, vijana ndio kundi kubwa zaidi ambalo hatma ya nchi ipo mikononi mwao.
Rais amehoji kwa kejeli kuwa kutokana na kuingiliana kwa jamii za Bara na Zanzibar kupitia ndoa, wazo la kuvunja Muungano halitekelezeki kwani lingemaanisha kuwatenganisha watoto waliozaliwa na pande zote mbili.
Aidha, Rais Samia amehimiza jumuiya ya UVCCM kusimamia kwa uadilifu miradi ya kiuchumi wanayobuni ili kukuza mapato ya jumuiya hiyo na kutengeneza urithi wa kudumu kwa vizazi vijavyo. Amewaahidi kuwa serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili vijana na kuwajengea uwezo wa kiuchumi kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo na Ilani ya CCM, akisisitiza kuwa viongozi wa sasa wanatayarisha mazingira bora kabla ya kuwakabidhi vijana kijiti cha uongozi wa nchi hapo baadaye.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment