" Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe Akutana na Rais wa Senegal

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe Akutana na Rais wa Senegal

 

Rais wa Shirikisho la soka Afrika, Patrice Motsepe, amesema atakaribisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa ndani ya Shirikisho hilo, akisema hawana la kuficha. Hii ilikuwa baada ya mkutano na Maafisa wa Senegal mjini Dakar.

Serikali ya Senegal imetaka uchunguzi ufanyike kuhusu ufisadi baada ya CAF kuamuru nchi hiyo kupokonywa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 na kuwapa Morocco ambao walikuwa washindi wake wa Fainali.

Patrice Motsepe alikutana na maofisa wa Shirikisho la soka la Senegal (SFF) na Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye siku ya Jumatano, ambapo alitoa wito wa umoja baada ya fainali.

Anatarajiwa kusafiri hadi Morocco siku ya Alhamisi kwa mikutano zaidi kama hiyo.

Motsepe pia alitupilia mbali pendekezo lolote kwamba Morocco ilipendelewa kuliko timu nyingine katika suala la kukata rufaa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post