" SACP MAGOMI ATAKA WANANCHI WADUMISHE AMANI SHINYANGA

SACP MAGOMI ATAKA WANANCHI WADUMISHE AMANI SHINYANGA

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani na kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika.

Akizungumza kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Aprili leo 28, 2026, Kamanda Magomi amesema ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama ni silaha muhimu katika kupambana na vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza katika jamii.

Amesema mafanikio yaliyopatikana katika operesheni mbalimbali zilizofanywa mkoani humo yanatokana na ushirikiano huo, huku akisisitiza kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili kudhibiti uhalifu na kulinda amani iliyopo.

Kamanda Magomi amebainisha kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahalifu na wale wote wanaokiuka sheria, na kuwataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kufuata sheria na taratibu za nchi, akieleza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kujenga mazingira salama na yenye utulivu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeendelea kutoa wito kwa jamii kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, kwa kushirikiana na mamlaka husika ili kuifanya Shinyanga kuwa sehemu salama kwa wote.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post