Msanii mkongwe wa muziki wa asili Saida Karoli
amefunguka kwa hisia kali katika kipindi cha Misalaba Media, akieleza maumivu
aliyopitia baada ya kumpoteza mama yake, hatua iliyomtikisa kisaikolojia na
kumfanya kupoteza mwelekeo wa maisha kwa kipindi fulani.
Pia Saida mbali na Mama yake amesema baada ya Ruger
kufariki, alijihisi kupoteza kila kitu kwani alikuwa nguzo muhimu katika maisha
na kazi yake ya muziki. Kutokana na hali hiyo, aliamua kurudi kijijini na
kujitenga na tasnia, huku akidai kuwa hata mawasiliano na wasanii wenzake
yalikatika kabisa.
Aidha, Saida aligusia changamoto nyingine ikiwemo
madai ya kuzushiwa mahusiano na bosi wake yaliyomuumiza zaidi, pamoja na
kueleza namna muziki unavyomchanganya kihisia anapokuwa peke yake.
Pia amedai kuwa msanii Diamond Platnumz aliwahi
kuwasiliana naye kuomba kutumia wimbo wake wa Salome, lakini baadaye
wimbo huo ulitoka bila makubaliano ya kifedha.
Licha ya kuitwa Malkia wa muziki wa asili, Saida
amesema bado anakabiliwa na maisha magumu, na amemuomba Rais Samia Suluhu
Hassan kumsaidia kupata bendi yake ya muziki.
Hata hivyo, ameweka wazi ndoto yake ya kufanya kazi na
Ali Kiba, hasa kwa kuurudia upya wimbo wake maarufu wa Salome.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment