MWANDISHI WETU, DODOMAWaziri wa Maji, Jumaa Aweso ameeleza kutofurahishwa na upotevu wa maji katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu huku baadhi wa wananchi wakikosa huduma hiyo muhimu.Waziri Aweso ameyasema hayo Aprili 15, 2026, katika uzinduzi wa Bodi ya 10 ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA). Akizungumzia suala hilo kwa hisia kali, Aweso amesema Mamlaka hiyo inapaswa kuchukua hatua za haraka kupunguza upotevu wa maji ambapo kwa sasa umefikia asilimia 33, jambo linaloitia hasara serikali kwa kupoteza mapato mengi."Niwaombe sana watendaji wote wa sekta ya maji, tudhibiti upotevu wa maji, mwananchi hawezi kukuelewa akiwa anakosa maji halafu anasikia kuna upotevu mkubwa wa maji," amesema Aweso.Sambamba na hilo, Aweso amesisitiza kuwa kipimo kimojawapo cha utendaji (KPI) kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji ni kudhibiti upotevu wa maji, kwani jambo hili linarudisha nyuma jitihada za usambazaji wa maji kwa wananchi.Katika hatua nyingine, Aweso amesema tabia ya baadhi wa watendaji na watumishi wasio waaminifu kwa kushiriki vitendo vya wizi wa maji kwa kuwaunganishia maji baadhi ya wateja katika hoteli na viwanda, bila kuwaingiza katika mifumo ya malipo, jambo linaloikosesha serikali mapato.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment