Wekundu wa Msimbazi Sc imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Leo April 15, 2026 kwenye Dimba la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Bao la kwanza limefungwa na Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama alipoachia mkwaju katika dakika za nyongeza (45+6) uliomshinda Machupa Kapili na kufunga bao lake la kwanza msimu huu katika ligi akiwa na uzi wa Wekundu hao wa msimbazi.
Baada ya kuwa mbele kwa bao 1-0, Simba ilirejea kipindi cha pili na kuonekana kuwa na utulivu zaidi katika eneo la mwisho, jambo lililowafanya vijana hao wa Steve Barker kupata bao la pili katika dakika ya 53 ambalo lilifungwa na Libasse Gueye kufuatia asisti ya Seleman Mwalimu.
Katika dakika ya 65, Simba ilifanya mabadiliko mawili kwa mpigo ikiwa ni mabadiliko yao ya tatu katika mchezo huo, walitolewa Mwalimu na Clement Kibabage huku wakiingia Anthony Mligo na Elie Mpanzu, awali aliingia Inno Loemba kuchukua nafasi ya Neo Maema.
Wakati Simba ikiwa mbele kwa mabao hayo, iliendelea kucheza kwa kujiamini huku ikitengeneza presha kubwa zaidi ya mashambulizi ambayo ilizaa matunda na kupata bao la tatu ambalo Shabani Pandu alijifunga.
Baada ya kuwa mbele kwa mabao 3-0, Barker aliamua kufanya mabadiliko mengine mawili kwa mpigo kwa kuwapa nafasi ya Hussein Mbegu na Morice Abraham wakichukua nafasi ya Rushine De Reuck na Chama.
Matokeo hayo yameifanya Simba ambayo imeendelea kuwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 39 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, kupunguza tofauti ya pointi kati yao na vinara, Yanga kutoka nane hadi tano.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment