Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media, Arusha.
Mkuu wa wilaya Arusha Joseph Mkude amesisitiza matumizi sahihi na utunzaji wa vyombo vya moto vilivyozinduliwa leo katika viwanja vya ofisi za TANESCO Jijini Arusha ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya umeme.
Akizindua vyombo hivyo ambavyo ni magari makubwa ya mitambo mawili, magari madogo manne, na bajaji tano amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuleta tija kwa wananchi, kila kitongoji kufikiwa na huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030.
"Ni tumaini letu kuwa, umeme unaenda kuwaka vitongoji vyote vya mkoa wa Arusha, vyombo hivi vikatumike kama hatua hiyo itaunga mkono jitihada za serikali yetu ya awamu ya sita" amesema Mkude.
Hata hivyo amepongeza maboresho makubwa yanayoendelea kufanywa na shirika la TANESCO Arusha usiku na mchana kuhakikisha kila mwananchi anafurahia huduma.
Katika namna hiyohiyo Meneja wa Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Arusha Eng.Kisika Kisika amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026 shirika limefanikiwa kuunganisha wateja wapatao 7580 na kufanya jumla ya wateja kuwa 318,869.
Vilevile amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 serikali imetenga kiasi cha TZS 19,058,149,786.00, katika kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme mkoa wa Arusha, utekelezaji wa miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali.Sambamba na hayo Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa jumla TZS 99,193,068,282.30.
"Kipekee naishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza miradi mikubwa ya umeme itakayochochea ukuaji wa uchumi na Taifa letu, pia tunashukuru uongozi wa serikali na chama mapinduzi katika mkoa wa Arusha kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku" amesema Eng.Kisika.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment