
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo vitaendelea kubaki katika hali ya utayari mkubwa Mashariki ya Kati, hata wakati mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Marekani na Iran yakitarajiwa kuanza rasmi.
Kupitia ujumbe wake, Trump alisisitiza kuwa meli za kivita, ndege za kijeshi pamoja na wanajeshi wa Marekani wataendelea kuwepo katika maeneo ya karibu na Iran, wakisubiri kuona kama makubaliano yatakayofikiwa yataheshimiwa kikamilifu.
Alionya kuwa endapo Iran haitazingatia makubaliano hayo, hatua kali zaidi za kijeshi zitachukuliwa, akisema mashambulizi yanaweza kuwa makubwa kuliko yale yaliyoshuhudiwa katika kipindi cha wiki sita tangu kuanza kwa mgogoro huo.
Rais wa Marekani, Donald Trump akiongea jambo akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth (Kushoto).
Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, aliunga mkono msimamo huo akieleza kuwa jeshi litaendelea kuwa macho muda wote, likiwa tayari kujilinda au kushambulia wakati wowote itakapohitajika.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika nchini Pakistan, yakiongozwa na viongozi waandamizi wa Marekani akiwemo Makamu wa Rais JD Vance pamoja na wajumbe wengine maalum wa kidiplomasia.
Hata hivyo, hali ya usitishaji vita bado inaonekana kuwa tete, hasa kutokana na changamoto zinazoendelea katika ufunguzi wa njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta ya Strait of Hormuz.
Ripoti zinaonesha kuwa idadi ya meli zinazopita katika lango hilo bado ni ndogo sana ukilinganisha na hali ya kawaida, jambo linaloashiria kuwa hali ya taharuki bado ipo licha ya juhudi za kurejesha amani.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanasema kuwa hatua ya Marekani kuweka jeshi katika hali ya utayari huku ikiendelea na mazungumzo inaonesha mkakati wa “diplomasia yenye nguvu ya kijeshi,” ambapo mazungumzo yanafanyika sambamba na maandalizi ya vita
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment