Na Mapuli Kitina Misalaba
Viongozi wa dini katika Kanisa la AICT Kambarage,
mkoani Shinyanga, wamewataka waumini kuendelea kudumisha amani na kuliombea
taifa ili kuimarisha umoja na mshikamano wa Watanzania.
Akifungua ibada hiyo, Mchungaji wa Kanisa la AICT
Kambarage, Charles Lugembe, amewataka Wakristo kumshukuru Mungu kwa amani
iliyopo nchini, akieleza kuwa hali hiyo imewezesha uhuru wa kuabudu kuendelea
kudumu bila vikwazo.
Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa waumini kuendelea
kuliombea taifa ili kudumisha hali ya utulivu na mshikamano, huku akibainisha
kuwa amani ni tunu inayopaswa kulindwa na kila Mtanzania.
Kwa upande wake, Mchungaji mstaafu Amos Ndaki ametumia
nafasi hiyo kuwaombea viongozi wa serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Waziri Mkuu na viongozi
wengine, ili waendelee kuliongoza taifa kwa hekima, amani na utulivu.
Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Askofu wa AICT Dayosisi
ya Shinyanga, Askofu Zakayo Bugota, na kupambwa na uimbaji wa kwaya mbalimbali
zikiwemo AIC Kambarage Choir, kwaya ya vijana, AIC Shinyanga pamoja na kwaya ya
akina mama.
Kwa pamoja, viongozi hao wa dini wamehimiza jamii kuendelea kuthamini na kulinda amani iliyopo nchini kama msingi wa maendeleo na ustawi wa taifa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment