" WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA APONGEZA UWAJIBIKAJI BORA WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA APONGEZA UWAJIBIKAJI BORA WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU


Na Egidia Vedasto,Misalaba Media, Arusha.Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amewapongeza wanasheria kwa uwajibikaji wao mahiri unaozingatia misingi na miongozo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hatua inayochochea maendeleo ya taifa.Amesema hayo jijini Arusha wakati wa mkutano wa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano, bidii, na kubadilishana maarifa ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao.Aidha, Dkt. Homera amepongeza hatua zilizochukuliwa katika kuboresha maslahi ya watumishi hao, sambamba na hayo amewataka waimarishe utendaji kazi, wadumishe mshikamano, pamoja na  kushughulikia mikataba kwa wakati.“Maendeleo ya taifa letu yanawategemea sana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ni wazi kuwa kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050, ni lazima tuhakikishe Wanasheria wetu wanapata mafunzo ya ndani na nje ya nchi. Nawaahidi nitaendelea kutoa vibali ili mkajinoe na kuongeza maarifa, hasa ikizingatiwa kuwa bajeti yetu imeongezeka,” amesema.Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Saidi Johari, amewataka watumishi kuyazingatia na kuyafanyia kazi yote yatakayojadiliwa katika mkutano huo muhimu.Amesema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu itaendelea kujenga ofisi katika mikoa mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa karibu na kwa wakati.“Kila mmoja ni shahidi kuwa Wanasheria wanafanya kazi katika mazingira safi, muonekano wao unadhihirisha kuwa maslahi yao yameboreshwa, na ninawaahidi kuwa tutaendelea kuboresha zaidi kwa lengo la kutoa huduma bora katika mazingira rafiki,” amesema.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post