" BUNGE LAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 359.3 YA WIZARA YA MAMBO YA NJE

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 359.3 YA WIZARA YA MAMBO YA NJE



Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya shilingi 359,326,404,000 kwa ajili ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2026/2027, baada ya kujadili na kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo.

Akiwasilisha makadirio hayo bungeni, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, aliliomba Bunge kuidhinisha fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Wizara katika mwaka ujao wa fedha.

Waziri Kombo alieleza kuwa kati ya fedha hizo, shilingi 312,961,378,000 zitatumika kwa Matumizi ya Kawaida, huku shilingi 46,365,026,000 zikitengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Baada ya mjadala wa wabunge, Bunge lilipitisha rasmi bajeti hiyo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kidiplomasia, ushirikiano wa kikanda na kimataifa pamoja na utekelezaji wa majukumu mengine ya Wizara.

Katika hotuba yake ya bajeti, Waziri Kombo alisema Tanzania imeendelea kudumisha misingi ya uhusiano na ushirikiano wa kimataifa kama ilivyowekwa na waasisi wa Taifa na kubainishwa katika Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001, Toleo la 2024.

Alitaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na kulinda mamlaka kamili ya nchi, mipaka na uhuru wa kisiasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kulinda haki za binadamu, usawa na demokrasia, kukuza ujirani mwema, kuimarisha Umoja wa Afrika, pamoja na kuongeza ushirikiano wa kiuchumi na washirika wa maendeleo.

Aidha, alisema Tanzania itaendelea kuunga mkono Umoja wa Mataifa katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi, amani na usalama duniani sambamba na kulinda maadili, mila na utamaduni wa Watanzania.

“Misingi hii imechangia kudumisha heshima na taswira njema ya Taifa letu kupitia ushirikiano wa uwili, kikanda na kimataifa,” alisisitiza Balozi Kombo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post