Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti, kimezindua matawi mapya 20 ya chama hicho katika kata tano za jimbo la Kahama Mjini, mkoani Shinyanga.Katibu wa Chadema wilaya ya Kahama (Msalala, Kahama Mjini na Ushetu) Samuel Peter amesema uzinduzi wa matawi hayo unalenga kurejesha shughuli za kichama, kusogeza huduma za chama kwa wananchi na kurejesha uhai wa chama hicho katika ngazi za chini.Peter amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla kuyatumia matawi hayo kuwasilisha kero na changamoto zao ili zitafutiwe ufumbuzi wa haraka.Amewahimiza viongozi wa matawi kushirikiana na wananchi kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano ndani ya chama, na kusisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa.Matawi hayo yamezinduliwa rasmi katika kata ya Mhongolo, Kahama Mjini, Majengo, Zongomela na Nyahanga."Leo tulikuwa na operesheni ya maandalizi ya mkutano mkubwa na wa kihistoria hapa Kahama utakaofanyika hapo kesho kwenye viwanja vya Fantom, Manispaa ya Kahama." Amesema na kuongeza "Wananchi wote tunawaalika kuhudhuria mkutano huu, viongozi wa kitaifa wa Chama watakuwepo, sio mkutano wa kukosa kabisa."Wakati huo huo Makamu mwenyekiti wa Chadema Zanzibar Said Mzee ameongoza kikao cha ndani cha baraza la uongozi wa kanda - Chadema, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho Taifa akiwemo katibu mkuu wa Chadema John Mnyika.Mambo mbalimbali ya kisiasa yamejadiliwa, ikiwemo mikakati ya kuendelea kuimarisha chama pamoja na kuongeza ushiriki wa wananchi katika shughuli za kisiasa na maendeleo ya jamii.Kwa upande wao baadhi ya wanachama waliohudhuria hafla hiyo wameeleza kufurahishwa na hatua ya uzinduzi wa matawi hayo, na kwamba yatasaidia kuongeza uhai wa Chama pamoja na kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi na wanachama wao.Shughuli hiyo imefanyika katika mazingira ya hamasa kubwa huku viongozi wa chama wakieleza kuwa CHADEMA itaendelea kuimarisha matawi yake katika Kanda ya Serengeti na kanda zingine, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya shughuli mbalimbali za kisiasa na maendeleo.Shughuli hizo zinafanyika siku moja kabla ya kuelekea mkutano wa hadhara wa CHADEMA, unaotarajiwa kufanyika kesho Mei 18,2026 katika viwanja vya Fantom Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, ukiwa na ujumbe wa 'Free Tundu Lissu' na 'Katiba Mpya '.Mwisho.
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Mzee akipandisha bendera ya chama hicho kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la Chama hicho, katika kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


















Post a Comment