Na Mapuli Kitina Misalaba
Ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 inayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeendelea kushika kasi huku timu ya Wafukunyungu FC kutoka mjini Shinyanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa leo dhidi ya Mwasenge kutoka kata ya Salawe.
Mashindano hayo ambayo yameanza rasmi Mei 16, 2026
yanashirikisha jumla ya timu 22 kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa
wa Shinyanga ikiwemo Mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Geita, Manispaa
ya Shinyanga pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga jimbo la Solwa.
Katibu wa kamati ya mashindano hayo amesoma ratiba ya
mechi za kesho ambapo DUARA FC watamenyana na MWANDUTU huku akiwahimiza
wananchi na wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kuendelea kushuhudia burudani
ya soka pamoja na vipaji vya vijana vinavyoendelea kuoneshwa katika mashindano
hayo.
Kwa upande wake mwandaaji wa mashindano hayo Bwana
Paul Daud maarufu MC NIACHEKONA amesema mshindi wa kwanza katika ligi hiyo
atazawadiwa zaidi ya shilingi milioni moja na nusu pamoja na kombe, huku
mshindi wa pili akitarajiwa kupata shilingi laki sita na mshindi wa tatu laki
tatu.
Aidha amesema kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa timu
na wachezaji watakaofanya vizuri ikiwemo timu yenye nidhamu, mchezaji bora
pamoja na golikipa bora wa mashindano hayo.
Mbali na michezo, MC NIACHEKONA ni Meneja wa Kishushu
Hotel na pia ni mchimba madini katika mgodi wa Mwakitolyo. Kwa huduma za MC
NIACHEKONA wasiliana naye kupitia namba 0757 267 738.
RATIBA YA MECHI – NIACHEKONA CUP 2026
Mei 16, 2026
HOME BOYS Vs MANHEIGANA
Mei 17, 2026
WAFUKUNYUNGU FC Vs MWASENGE
Mei 18, 2026
DUARA FC Vs MWANDUTU
Mei 19, 2026
SHILIMA Vs SONGAMBELE MHANGU
Mei 20, 2026
NYUNDO FC Vs NZOZA
Mei 21, 2026
MAHEMBE Vs MAWEMIRU
Mei 22, 2026
NYANDOLWA Vs BAJAJ FC
Mei 23, 2026
SHILABELA Vs LYABUKANDE
Mei 24, 2026
KIMANDAGULI Vs KASHISHI
Mei 25, 2026
ISENENGEJA Vs MWAKITOLYO No.6
Mei 26, 2026
SANGU FC Vs BULIGE
Mazoezi kabla ya mechi
Mchezo ukiendelea katika uwanja uliopo kijiji cha Mwabenda huku timu zikioneshana uwezo mkubwa dimbani.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






















Post a Comment