" CHAMA AIPA YANGA PRESHA MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU

CHAMA AIPA YANGA PRESHA MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU



Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Mei 14, 2026, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Mabao ya Simba SC yalifungwa na Clatous Chama dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza na dakika ya 69 ya kipindi cha pili, huku bao la tatu likifungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 90+2 na kuifanya timu hiyo kuondoka na pointi tatu muhimu.

Kwa ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi 52 ikiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, huku watani zao Young Africans SC wakiendelea kuongoza ligi kwa pointi 54, huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 23.

Post a Comment

Previous Post Next Post