
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujipatia zaidi ya Shilingi 81,500,000 kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao wa utapeli wa ajira uliokuwa ukilenga vijana wanaotafuta nafasi za kazi ndani na nje ya nchi.
Watuhumiwa hao walikamatwa Mei 14, 2026 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya, wakihusishwa na kuwashawishi vijana kwa madai ya kuwapatia ajira kupitia kampuni zinazodaiwa kuwa za Q NET na Global Alliance.
Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakiwahadaa vijana kutoa fedha kuanzia Shilingi 40,000 hadi kufikia Shilingi milioni tano kwa kila mtu, wakiahidi kuwapatia nafasi za ajira nje ya nchi kupitia kampuni hizo, jambo ambalo baadaye lilibainika kuwa la uongo.
Zaidi ya vijana 80 kutoka maeneo mbalimbali nchini waliaminishwa na kuingia katika mtego huo, ambapo walikusanywa katika nyumba zilizopo maeneo ya Iwambi, Shewa, Isyesye na Iyunga jijini Mbeya na kutoa fedha kwa matarajio ya kupata ajira.
Watuhumiwa waliokamatwa ni William Hamis wa Mwambene, Tyson Lubida wa Shewa, Onesmo Hildepbonce wa Isyesye, Charles Masanja wa Iwambi, Chemka Mwanyanga wa Iwambi, Gracia Ephraim wa Isyesye pamoja na Ezekiel Mgogo wa Igunga mkoani Tabora.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetoa wito kwa wananchi hususan vijana wanaotafuta ajira kuepuka kurubuniwa na watu wanaodai kutoa ajira kwa malipo, ukisisitiza kuwa ajira rasmi hazihitaji malipo ya aina hiyo na kuwataka kufuata njia rasmi za kupata taarifa za ajira.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment