Na: Belnardo Costantine.Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi la polisa Tanzania CP Awadhi Juma Haji, amefunga rasmi mafunzo ya medani za kivita yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) kambi ya Mkomazi, Mkoani Tanga.Aidha Kamishna Awadhi amewataka Askari walioshiriki mafundi hayo kudumisha Nidhamu, kufuata Sheria, kanuni na taratibu za nchi Sambamba na kuyaishi kwa vitendo mafunzo waliyoyapata popote watakapokwenda Katika kutekeleza majukumu yao .Hata hivyo amesema ni muhimu Kila mmoja kuhakikisha analinda heshima ya Jeshi la Polisi popote alipo bila kujalii yupo kazini au yupo kwenye shughuli binafsi.Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, DCP Dkt. Lazaro Mambosasa, amemhakikishia Kamishna kuwa, maelekezo aliyoyatoa yatasimamiwa na kutekelezwa ipasavyo ili kuleta tija ndani ya Jeshi la Polisi kwa kuwa na Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wenye weledi na uwezo wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment