Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe.Denis Masanja, leo Mei 25, 2026 amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kalonga kilichopo Kata ya Mlingoti Magharibi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.Katika mkutano huo, DC Masanja amepata fursa ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi pamoja na kutoa maelekezo kwa wataalamu na viongozi wa maeneo husika kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.Akizungumza na wananchi wa Kalonga, Mheshimiwa Masanja amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule na kuhakikisha wanandikishwa kwa wakati ili kupata haki yao ya msingi ya elimu.Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kuilinda na kuidumisha amani iliyopo katika Wilaya ya Tunduru na Tanzania kwa ujumla, akieleza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya wananchi na taifa.Katika hatua nyingine, DC Masanja ametoa rai kwa wananchi kuzingatia matumizi bora ya ardhi pamoja na kutunza mazingira yanayozunguka kijiji chao ili kuepuka milipuko ya magonjwa na kulinda afya za jamii.Pia amewataka wakulima kuepuka kuuza zao la ufuta kupitia mifumo isiyo rasmi maarufu kama “Kangomba” na badala yake kutumia mfumo wa Stakabadhi Ghalani, ambao unalenga kuhakikisha wakulima wanapata soko la uhakika, bei nzuri pamoja na kulinda maslahi yao kupitia mfumo rasmi wa uuzaji wa mazao.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















Post a Comment