Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, Evarist Simon Mnyere, ameongoza
maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi yaliyofanyika Wilaya ya Mpanda Mei
7, 2026, huku akisisitiza umuhimu wa malezi bora na uzalendo katika kujenga
taifa imara.
Katika
maadhimisho hayo yaliyowakutanisha viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi
kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, Mnyere alisema wazazi wana wajibu mkubwa
wa kushirikiana katika malezi ya watoto na vijana ili kuhakikisha jamii inapata
viongozi bora wa baadaye.
Akizungumza
katika hafla hiyo, aliwahimiza wazazi kuwaunganisha watoto katika ngazi
mbalimbali za elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati hadi vyuo
vikuu, kwa lengo la kuwajengea misingi ya maadili, uzalendo na uwajibikaji.
Aidha,
alisisitiza umuhimu wa wazazi kushiriki shughuli za maendeleo na malezi mema
katika jamii huku wakitekeleza kwa vitendo sera za malezi na makuzi ya watoto.
Mnyere pia
aliwataka wazazi kuendelea kutunza mazingira, kuzingatia masuala ya afya,
pamoja na kuimarisha maadili ya taifa kwa kuendeleza umoja na mshikamano ndani
ya jumuiya hiyo.
Katika hatua
nyingine, aliwashukuru wanachama wa Jumuiya ya Wazazi pamoja na viongozi wa
chama na serikali kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuimarisha jumuiya hiyo na
kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Pia
aliwahimiza wanachama kuendelea kubuni miradi ya maendeleo, kufanya mikutano ya
mara kwa mara, kuweka takwimu sahihi za wanachama na kuimarisha nidhamu pamoja
na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa isemayo, “Malezi Bora na Uzalendo ni Msingi wa Taifa,” ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kuwekeza katika maadili na malezi ya watoto kwa maendeleo ya taifa.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi, amewasili na kuwasalimia wanachama pamoja na wananchi katika eneo la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, akiwa katika mwendelezo wa shughuli za maadhimisho hayo.
Ndg. Dr. Patrick, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, akiwa pamoja na Ndg. Mushi, Katibu wa Hospitali hiyo, wameongoza viongozi na wageni mbalimbali kutembelea na kukagua maeneo ya Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na mgeni rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi yaliyofanyika Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, akiwasili katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa ajili ya kujulia hali wagonjwa, kupanda miti ya matunda na kivuli pamoja na kutoa misaada kwa wagonjwa.

Ndg. Taus, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mpanda, akishiriki kikamilifu maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi yaliyofanyika Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Nsimbo.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi, amewasili katika eneo la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, akiwa katika mwendelezo wa shughuli za maadhimisho hayo.
Ndg. Aziza Said Self, Katibu wa UWT Wilaya ya Mpanda, akiwasalimia viongozi katika kikao cha pamoja kilichofanyika wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mpanda.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na mgeni rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi yaliyofanyika Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Nsimbo, akipata maelekezo kutoka kwa madaktari wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi katika Wilaya ya Mpanda (Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo), ameungana katika picha ya pamoja na madaktari wakati wa maadhimisho hayo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi na sekta ya afya katika kuendeleza huduma kwa jamii.
Ndg. Sophia, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi, akiwasalimia na kuwakaribisha wajumbe katika maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi yaliyofanyika Wilaya ya Mpanda, ambapo pia alisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano katika kuijenga Jumuiya ya Wazazi.
Ndg. Taus, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mpanda, akishiriki kikamilifu maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi yaliyofanyika Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Nsimbo.

Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, akiwasalimia na kuwashukuru wajumbe waliohudhuria maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi yaliyofanyika Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Nsimbo, huku akisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu ya kila kiongozi kwa ufanisi na weledi.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi katika Wilaya ya Mpanda (Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo), ameungana katika picha ya pamoja na madaktari wakati wa maadhimisho hayo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi na sekta ya afya katika kuendeleza huduma kwa jamii.
Ndg. Evarist Simon Mnyere, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi na Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi katika Wilaya ya Mpanda (Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo), ameshiriki kikamilifu zoezi la upandaji miti ya matunda na miti ya kivuli kwa lengo la kuimarisha mazingira na kuongeza uoto wa asili.
Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, ameshiriki kikamilifu katika shughuli na vikao mbalimbali vya Jumuiya ya Wazazi CCM vinavyoendelea ndani ya Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.
MPANDA — Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi na mwenyeji wa ugeni katika maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi, ameshiriki kikamilifu maadhimisho hayo akisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano ili kuhakikisha shughuli za Wiki ya Wazazi Mkoa wa Katavi zinaenda vizuri na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, ameshiriki kikamilifu katika shughuli na vikao mbalimbali vya Jumuiya ya Wazazi CCM vinavyoendelea ndani ya Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254











Post a Comment