Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye amewataka wanafunzi wanaoshiriki mashindano ya UMITASHUMTA 2026 ngazi ya Mkoa ambao ni wawakilishi wa Halmashauri hiyo kushirikiana kila wakati kujituma na kudumisha nidhamu kwa kuzingatia maelekezo wanayopewa ili kupata nafasi ya kuchaguliwa kuunda timu ya Mkoa wa Kigoma.Mwl. Simbeye amesema hayo baada ya kutembelea kambi ya wachezaji hao iliyopo katika Shule ya Sekondari Bongwe huku akiwakumbusha juu ya umuhimu wa michezo katika kuimarisha afya na kufungua fursa za mbalimbali za ajira.Aidha, ameahidi kuendelea kuwapa ushirikiano katika kipindi chote cha mashindano hayo ngazi ya Mkoa yanayoanza rasmi tarehe 28 hadi 31 Mei 2026.Kwa sasa timu zote kutoka Halmashauri mbalimbali Mkoani Kigoma zimeweka kambi katika Shule ya Sekondari Bongwe zikiendelea na maandalizi kuelekea michezo ya kuteua wachezaji watakaounda timu ya Mkoa itakayoenda kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa Mkoani Njombe.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254










Post a Comment