Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amepokea taarifa inayohusu masuala mbalimbali ya sekta ya ardhi katika Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma.Taarifa hiyo imewasilishwa mapema leo, Mei 17, 2026, na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Col. Isaac Anthony Mwakisu, akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.Katika muendelezo wa ziara hiyo, Mhe. Mmuya anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Zeze leo, kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zao za ardhi. Hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayetaka viongozi na watendaji kuwafuata wananchi maeneo yao ili kutatua kero zinazowakabili.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment