Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameiomba Taasisi ya Global Partnership for Education (GPE) kuendelea kuongeza ufadhili wa miradi ya elimu mkoani humo ili kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, hasa katika maeneo yenye changamoto kubwa ikiwemo Wilaya ya Ukerewe.
RC Mtanda ameyasema hayo alipokutana na kufanya kikao kifupi na Bw. Morten Sigsgaard pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Sweden, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na TAMISEMI waliowasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwa kupitia GPE katika Wilaya za Ilemela, Sengerema na Ukerewe kuanzia Mei 11 hadi 13, 2026.
Amesema Mkoa wa Mwanza bado una uhitaji mkubwa wa nyumba za walimu, vifaa vya TEHAMA na miundombinu ya elimu hususani katika Wilaya ya Ukerewe kutokana na mazingira ya kisiwa yanayosababisha baadhi ya watumishi kukwepa kufanya kazi huko. Amesisitiza kuwa kuboresha mazingira ya kazi kutasaidia kuongeza morali na ufanisi kwa walimu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Mwl. Aisa Rupia, Mkoa umepokea zaidi ya Shilingi bilioni 1.9 kupitia mradi wa GPE-TSP tangu mwaka 2023/2024 hadi 2025/2026 kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu katika halmashauri zote nane za Mkoa huo.
Miradi iliyotekelezwa kupitia ufadhili huo ni pamoja na ujenzi wa madarasa 23, vituo 8 vya rasilimali za walimu (TRCs), matundu 30 ya vyoo pamoja na nyumba 10 za walimu. Aidha, mradi huo umechangia kuimarisha uwezo wa walimu kupitia mafunzo, semina na programu za maendeleo endelevu ya taaluma ya ualimu.
Katika sekta ya TEHAMA, shule na vituo vya walimu vimepatiwa kompyuta 200 za mezani, laptop 21, mashine 19 za kunakili nyaraka, kamera 9 za kidigitali, projectors 17 pamoja na skrini 16 za maonesho kwa ajili ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa matokeo ya elimu yameendelea kuimarika ambapo ufaulu wa Darasa la Saba umeongezeka kutoka asilimia 84.72 mwaka 2023 hadi asilimia 91.66 mwaka 2025, huku ufaulu wa Kidato cha Nne ukiongezeka kutoka asilimia 93 mwaka 2023 hadi asilimia 98.66 mwaka 2025.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment