" RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA VYATAJWA KUATHIRI MAENDELEO YA VIJANA

RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA VYATAJWA KUATHIRI MAENDELEO YA VIJANA

 

Na Edington Mukiza Ezron, Misalaba Media

Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga wamewataka viongozi wa serikali kuwa waadilifu na kupambana na rushwa ili kudhibiti usambazaji wa dawa za kulevya, ikiwemo kilimo cha bangi, sambamba na kuongeza fursa za ajira kwa vijana ili kupunguza utegemezi na kuimarisha ustawi wao wa kiuchumi.

Wametoa wito hu oleo Mei 1, 2026 wakati wakizungumza na Misalaba Media ambapo pia wamewasisitiza vijana kudumisha maadili, kuwa wachapakazi na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini ili kujikwamua kiuchumi na kuepuka kujiingiza katika vitendo visivyofaa.

 

Akizungumza Abdallah Hassan, mkazi wa Ndala, amesema vijana wanapaswa kujishughulisha na shughuli mbalimbali badala ya kusubiri ajira rasmi, huku akisisitiza umuhimu wa kuepuka makundi mabaya yanayoweza kuwashawishi kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya. Amesema vijana ni nguvu kazi muhimu ya taifa na wanapaswa kutumia ipasavyo fursa zinazojitokeza.

“Vijana wanatakiwa kutumia fursa zilizopo, mfano mashindano ya AFCON 2027 yanaweza kuwa chanzo cha ajira na kipato kwao,” amesema Hassan.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa vijana kutumia vyema utandawazi na teknolojia ya mawasiliano kwa kujifunza mambo yenye tija, badala ya kujiingiza katika vitendo vinavyokiuka maadili. Aidha, amesisitiza kuwa malezi si jukumu la wazazi pekee, bali ni wajibu wa jamii nzima kushirikiana katika kuwalea watoto.

Kwa upande wake, Hamis Hassan amesema wazazi wanapaswa kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu ili kuwaepusha na vitendo vya tamaa, pamoja na kuwajengea misingi imara ya kimaadili na kuwaelekeza kuepuka marafiki wabaya.

Naye Devotha Mfoyi amependekeza kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa watoto wanaoishi mitaani, pamoja na kuimarishwa kwa ukaguzi katika maeneo yanayohusishwa na biashara ya dawa za kulevya, huku wahusika wakichukuliwa hatua kali za kisheria.

Kitenge Hamad Chubwa amesema vijana wanahitaji kupewa elimu na ushauri kutoka kwa wazee na taasisi mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kifikra na kimaadili, jambo litakalowasaidia kuepuka vitendo viovu na kujenga taifa lenye nguvu na maadili imara.

Kwa upande wake, Leonard Dominick ameshauri kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na kushughulikia tatizo la watoto wanaozurura mitaani bila kwenda shule, akisisitiza kuwa viongozi wa serikali za mitaa wanapaswa kuchukua hatua kwa kuwa wanawafahamu wahusika.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post