
Na Milu Malimi, Misalaba Media
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wameeleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana, wakisema hali hiyo inaathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa maisha yao na maendeleo ya jamii.
Wakizungumza na Misalaba Media Mei 1, 2026, wananchi
hao wamesema matumizi ya dawa za kulevya yamechangia kuongezeka kwa vitendo vya
uhalifu ikiwemo uporaji, unyanyasaji wa watoto pamoja na kuvunjika kwa familia,
huku vijana wengi wakijikuta wakiingia katika makundi hatarishi na kushawishiwa
na marafiki wabaya.
Miongoni mwa waliozungumza ni Abdallah Rajabu, Hamis
Hasan, Devotha Mfoi na Kitenge Chubwa, ambao wameeleza kuwa ukosefu wa ajira
umeendelea kuwa sababu kubwa inayowasukuma baadhi ya vijana kujiingiza katika
matumizi ya dawa hizo, sambamba na ushawishi wa makundi rika yanayowavuta
kwenye vitendo vya kihalifu kama ujambazi na ukabaji.
Wamesisitiza kuwa wazazi na walezi wanapaswa
kuimarisha malezi kwa kuwafuatilia watoto wao kwa karibu na kujenga mazingira
ya mawasiliano ya wazi, ili vijana waweze kueleza changamoto wanazokutana nazo
kabla ya kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha, wamezitaka shule na taasisi mbalimbali kuongeza
juhudi za utoaji elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya, huku wakihimiza jamii
kuwajengea vijana uwezo kupitia mafunzo ya ujasiriamali na fursa nyingine za
maendeleo ili waweze kujitegemea.
Kwa upande mwingine, wananchi hao wameitaka jamii
kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa kuhusu wahusika wa biashara
haramu ya dawa za kulevya, wakiamini hatua hiyo itasaidia kujenga mazingira
salama na kulinda nguvu kazi ya taifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment