Wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi Mkoa wa Kigoma wametakiwa kuzingatia sheria za kazi na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu ili kuongeza tija na kuchochea maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro wakati akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Uvinza huku akisisitiza umuhimu wa waajiri kuhakikisha watumishi wanapatiwa stahiki zao kwa wakati.Balozi Sirro amewaonya watumishi wanaotumia muda wa kazi kwenda kwenye majukumu yao binafsi badala ya kuhudumia wananchi akibainisha kuwa jambo hilo linarudisha nyuma juhudi za Serikali za kuboresha huduma kwa wananchi.Awali, akisoma risala ya wafanyakazi Mkoa wa Kigoma Katibu wa TALGWU Mkoani humo Johnson Muyombya ameiomba Serikali kufanya maboresho ya sheria za wafanyakazi pamoja na kudhibiti waajiri wasiowajibika kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati.Katika hatua nyingine, Katibu Johnson amewasisitiza waajiriwa wote wa sekta za umma na binafsi kutekeleza majukumu yao kwa bidii na weledi sambamba na kupiga vita vitendo vya rushwa.Baadhi ya wafanyakazi waliohudhuria sherehe hizo wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria na taratibu zote za kazi ili kuboresha huduma kwa wananchi.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254










Post a Comment