" Simba SC vs Yanga SC : Ukipoteza ubingwa unasuasua

Simba SC vs Yanga SC : Ukipoteza ubingwa unasuasua

 

Simba SC vs Yanga SC ni mchezo unaofuata kwenye NBC Premier League, Mei 3, 2026 kwa wababe hawa kusaka pointi tatu muhimu.

Mohamed Hussen beki wa Yanga SC ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho una maana kubwa kutokana na kushikilia alama muhimu za timu kutwaa ubingwa wa NBC Premier League.

Yanga SC ni mabingwa watetezi, wanaongoza ligi wakiwa na pointi 47 huku Simba SC nafasi ya pili na pointi 42 tofauti ya pointi 5 pekee zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 19.

Mchezo wa kesho unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo saa 12:00 jioni kwa wababe hawa kusaka pointi tatu.

Zimbwe amesema: “Ukipoteza mchezo wa kesho maana yake kwenye mbio za ubingwa utakuwa una suasua, hivyo tunatambua umuhimu wa kushinda kesho ili tuongeze gap la alama kati yetu na mpinzani wetu.

“Kila mmoja anatambua ubora wa wapinzani wetu, lakini pia tunatambua ubora wetu, kwenye mapungufu yetu tunakwenda kuyafanyia kazi na kwenye ubora tunakwenda kuongeza, tuna amini kuwa tunakwenda kukusanya alama tatu hapo kesho,”.

Post a Comment

Previous Post Next Post