Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya TRA United katika mchezo wa kuisaka tiketi ya kufuzu nusu fainali ya CRDB Federation Cup uliopigwa kwenye dimba la KMC Complex, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 6, Anicet Oura dakika ya 26, Seleman Mwalimu dakika ya 64, pamoja na Bashir Kibaila dakika ya 78.

Kufuatia matokeo hayo, katika mchezo wa nusu fainali Simba SC watamenyana na Coastal Union, huku Young Africans SC wakicheza dhidi ya Azam FC.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254