Mwandishi wetuShinyangaKatibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Agnes Meena, ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa mchango wake mkubwa katika kuwezesha wafugaji kupitia utoaji wa mitaji na huduma za kifedha zinazochochea maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.Akifungua rasmi Maonesho ya Mifugo Kanda ya Ziwa 2026 yaliyofanyika Busanda, Shinyanga, Bi. Meena alisema uwekezaji wa TADB umechangia kuongeza uzalishaji, tija na ukuaji wa ufugaji wa kibiashara, huku akiitaka benki hiyo kuendelea kushirikiana na wadau wengine kutatua changamoto za wafugaji.Kwa mujibu wa TADB, benki hiyo tayari imetoa mikopo ya zaidi ya Shilingi Bilioni 119 kwa maendeleo ya sekta ya mifugo nchini, ambapo Shilingi Bilioni 25 zimetolewa katika Kanda ya Ziwa pekee.Uwekezaji huo umenufaisha zaidi ya Watanzania 60,000 na kuimarisha mchango wa sekta ya mifugo katika ukuaji wa uchumi wa taifa.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment