Abiria wa masafa marefu wamepatiwa elimu kuhusu kupaza sauti zao pindi wafanyiwapo au waonapo vitendo vya ukatili wa kijinsia vikitendeka ndani ya gari wawapo safariniAkitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewataka abiria kutokukubaliana na vitendo hivyo kufanyika wakiwa safarini kama utolewaji wa lugha za udhalilishaji, kushikwa maungo wanawake Kwa kisingizio Cha msongamano wa watu ndani ya gari, kupakatwa Kwa wanafunzi wa kike Kwa kisingizio Cha kukosa siti au kumdhalilisha mtu kulingana na umbo lake pia utolewaji wa lugha za vitisho.Aidha Sajenti Ndimila amewaeleza abiria kuwa mwili wa kila mtu ni wake, hakuna mtu mwenye haki ya kuugusa, kuuzungumzia au kumtumia kingono bila ruhusa yake kamili.Abiria wamesisitizwa kuwa kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie Kwa kupaza sauti zao na kuzuia vitendo hivyo Kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment