" TUMUUNGE MKONO DK. BATILDA BURIAN UJENZI KITUO CHA TIBA YA MOYO KCMC

TUMUUNGE MKONO DK. BATILDA BURIAN UJENZI KITUO CHA TIBA YA MOYO KCMC

NA: DK. REUBENI LUMBAGALA

Ugonjwa wa moyo ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza. Ni ugonjwa ambao kama Taifa tunapaswa kuchukua hatua madhubuti kwa kutoa elimu kwa wananchi juuu ya namna ya kujikinga na endapo mwananchi ataugua pasi pawepo na uhakika wa kupata matibabu yake.

Kwa sasa, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ndiyo inayotegemewa kwa kiasi kikubwa kuwatibu wagonjwa wa moyo hapa nchini. Kutokana na wingi wa wagonjwa wa moyo, taasisi hii inalemewa.

Si hivyo tu, wagonjwa wa moyo wanatoka mikoa mbalimbali, hivyo uwepo wa JKCI ya Jijini Dar es Salaam, kunaongeza gharama za kupata matibabu kwa kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu.

Kwa msingi huu, kuna kila sababu ya kuwa na taasisi nyingine za moyo nchini ili kurahisisha upatikanaji wa matibabu hasa kule walipo wananchi.

Jambo la kutia matumaini ni kwamba, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) imekuja na mpango kabambe wa ujenzi wa Kituo cha Tiba ya Moyo KCMC ili kutanua wigo wa upatikanaji wa huduma ya moyo.

Mei 25, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Burian alizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya tukio la uchangiaji kufanikisha ujenzi wa kituo hicho ambacho hadi kukamilika kwake kitagharimu shilingi bilioni 25. 

Hadi sasa KCMC wanazo shilingi bilioni 22 za ujenzi wa majengo na miundombinu mingine, ambapo fedha inayopaswa kuchangwa na wadau ni bilioni 3 ili kutimiza bilioni 25 za mradi huo muhimu hasa katika ununuzi wa vifaatiba. 

"Niwasihi wadau, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kujitokeza Mei 30 siku ya Jumamosi katika Hoteli ya Tanga Beach kushiriki hafla ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Moyo ya KCMC. Takwimu zinaonyesha asilimia 40 hadi 60 ya wagonjwa wa moyo wanatoka Kanda ya Kaskazini, kwahiyo, uwepo wa taasisi hii inasaidia sana kuwapunguzia gharama wananchi," amesema Dk. Burian.

Niwasihi wananchi wenzangu, kujitoa kwa hali na mali kuchangia ujenzi wa Kituo hiki cha Moyo KCMC. Wahenga walisema haba na haba hujaza kibaba. Shilingi bilioni 3 zinaweza kupatikana kwa haraka tukiunganisha nguvu kwa pamoja.

Pengine ni vizuri sasa, kuwa na njia rafiki za watu kuweza kuchangia fedha hasa kupitia akaunti namba za benki na namba za mitandao ya simu ili mwananchi aweze kuchangia alichonacho kule alipo hasa kwa wale watakaoshindwa kuhudhuria hafla hiyo.

Mei 30, wadau wajitokeze kwa wingi katika Hoteli ya Tanga Beach Resort, Jijini Tanga, kushiriki hafla hiyo muhimu ya kuchangia shilingi bilioni 3. Na kwa wale watakaoshindwa basi washiriki baraka hizo zenye thawabu kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya miamala ya kifedha katika simu zao.

Tukumbuke jambo hili jema si jambo la wananchi wa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara pekee, ni suala la kitaifa. Ni suala linalogusa maisha ya Watanzania wote na hata wasio Watanzania. Hata ndugu zangu Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) itapendeza kama watachangia.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post