Uundaji wa Tume za Kijaji nchini Tanzania umekuwa chombo muhimu na madhubuti cha kisheria kinachotumiwa na Wakuu wa Nchi pale kunapojitokeza malalamiko makubwa ya jamii, hasa yanayogusa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Historia inaonyesha kuwa tume hizi si ngeni na zimekuwa na mchango mkubwa katika kuleta uwajibikaji wa kiutawala na kisheria.
Mfano wa wazi ni uamuzi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye mwaka 2014 aliunda Tume ya Kijaji iliyojumuisha majaji wastaafu watatu,
Hamisi Amiri Msumi, Stephen Ernest Ihema, na Vincent Kitubio Damian Lyimo, ili kuchunguza madai ya mauaji na mateso yaliyosababishwa na Operesheni Tokomeza Ujangili iliyokuwa chini ya maelekezo ya Waziri wa Maliasili wa wakati huo, Balozi Hamisi Kagasheki.
Kazi ya tume hiyo ya kihistoria haikuishia kwenye makaratasi, kwani ilithibitisha uwepo wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kusababisha hatua kubwa za kiutawala kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na Waziri Kagasheki kupoteza nafasi yake ya uwaziri.
Hatua kama hizi zilionekana pia katika Tume ya Jaji Msemembo Mussa Kipenka iliyoundwa mwaka 2006 ikishirikiana na wajumbe wengine kama Mwantum Malale na Arthur Mwaitenda, kuchunguza vifo vya wachimba madini wanne huko Sinza jijini Dar es Salaam vinavyodaiwa kutekelezwa na jeshi la polisi.
Taarifa ya Tume hiyo ilionyesha ushiriki wa watuhumiwa katika mauaji hayo, ambapo Serikali ilichukua hatua za kijinai zilizopelekea baadhi ya watuhumiwa kuhukumiwa kunyongwa na mahakama, jambo linalothibitisha kuwa tume hizi zina nguvu na mafanikio makubwa katika kusimamia haki.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment