Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeendelea kuonyesha mafanikio katika ukusanyaji wa mapato baada ya kufanikisha kukusanya asilimia 87.79 ya mapato yaliyokadiriwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026. Mafanikio hayo yametajwa kuwa ishara ya kuimarika kwa usimamizi wa mapato pamoja na utekelezaji mzuri wa mipango ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.Mafanikio hayo yamejadiliwa katika Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Skyway, Wilaya ya Tunduru, ukiwa na lengo la kupitia mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo pamoja na mikakati ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Sefu Dauda, amesema mshikamano na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya ukusanyaji wa mapato yaliyofikiwa hadi sasa. Amesisitiza kuwa ushirikiano huo ni msingi muhimu katika kuharakisha maendeleo ya wilaya na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi.Aidha, Mhe. Dauda amesema halmashauri itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na kusimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora. Ameongeza kuwa ushiriki wa wananchi katika kulipa kodi na kuchangia shughuli za maendeleo utaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Wilaya ya Tunduru.Kwa upande wake,Afisa serikali za mitaa Ruvuma Amandus chilumba ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, akieleza kuwa hadi kufikia robo ya tatu halmashauri imefanikiwa kufikia asilimia 87.79% ya makusanyo. Amesema mafanikio hayo ni ishara ya uwajibikaji, usimamizi mzuri na mshikamano wa madiwani katika kuisimamia halmashauri hiyo. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuibua vyanzo vipya vya mapato pamoja na kudumisha amani, umoja na ushirikiano ili kuhakikisha maendeleo endelevu yanaendelea kupatikana kwa manufaa ya wananchi wote.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment