UJENZI wa madaraja matatu Jijini Mwanza kupitia ukandarasi wa Kampuni ya Jonta Investment Ltd umefikia asilimia 48 ya utekelezaji wake huku kasi ya kazi hizo ikiongezeka kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha kuanza kupungua kwa sasa.Akizungumza jana jijini hapa, Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoani Mwanza, Mhandisi Makori Kisare alisema kuwa kutokana na kupungua kwa mvua katika maeneo tofauti mkoani Mwanza ukamilishaji wa ujenzi wa daraja hizo zote utakamilika mwezi Ogasti mwaka huu.Aliwataka wananchi kuondoa hofu kutokana na habari potofu iliyosambazwa kuwa mkandarasi ameondoka kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa daraja katika barabara ya Uhuru na badala yake wafahamu kuwa alikuwa akitekeleza miradi yote mitatu ambayo kwa sasa imefikia asilimia 48."Mkandarasi huyu anajenga daraja mbili eneo la Kishiri Fumagila, Uhuru na Mlango Mmoja jumla mawili vilevile barabara hivyo alikuwa akiendelea maeneo mengine kufanya kazi"alisema Mhandisi Kisare.Mhandisi Kisare alisema mkoa ulipatiwa bilioni 23 kwa ajili ya miradi ya barabara ambapo asilimia 60 ya miradi inatekelezwa huku zilizobaki zinaendelea kujenga huku mkazo ukiwa ni kuhakikisha kuwa barabara zisizopitika zinafunguliwa na kupitika wakati wote.Naye Meneja wa TARURA wilayani Nyamagana Mhandisi Dunstan Kishaka alisema kuwa mkandarasi anayetekeleza kazi hiyo anayo maeneo mengine matatu anayojenga madaraja manne na barabara hivyo amekuwa akisimama kuendelea na kazi kutokana na kuongezeka kwa mvua.Alisema ujenzi wa daraja la Uhuru umekuwa ukisimama wakati mvua zilipokuwa zikizidi maana kuna muda maji yalisomba kila kitu kwenye eneo hilo kwa hiyo mkandarasi alianza kufanya kazi zake kwa uangalifu mkubwa ikiwa pamoja na kusimamisha kazi mvua inapozidi.Mhandisi Kishaka alisema daraja la Kishiri Fumagila limefikia asilimia 78, Mlango Mmoja 20 na Uhuru 35 huku likiwa limekamilika kuwekewa mguu mmoja na kesho wanaenda kujenga mguu wa pili ambapo gharama kwa miradi hiyo ni bilioni 1.49.Alisema vifaa kwa ajili kukamilisha mradi wa uhuru zimeletwa kwenye eneo la kazi wakati huo huo akiwa hajachukua malipo yote kwenye kazi zote ambapo ujenzi unafanywa kwa fedha toka benki ya dunia.Mhandisi Kishaka alisema ni utashi wa mkandarasi mwenyewe kutumia fedha zake bila ya kuomba fedha toka TARURA hivyo kuwapatia imani juu ya uwezo wa mkandarasi huyo mzalendo.Wahandisi hao waliwataka watumiaji wa barabara kutumia kwa uangalifu ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na hivyo kuwezesha serikali kutekeleza miradi mingine ya barabara sehemu zingine.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment