Habari njema kwa watumiaji wa mafuta nchini. Kuanzia Jumatano, tarehe 01 Julai 2026, bei kikomo za bidhaa za petroli zimeshuka kutokana na kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, imesema kutokana na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia, bei za mafuta katika soko la hapa nchini zinashuka kwa Shilingi 96 kwa lita ya petroli, Shilingi 151 kwa lita ya dizeli na Shilingi 242 kwa lita ya mafuta ya taa.
Kushuka huku kunatokana na mabadiliko katika soko la dunia, ikiwemo makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Marekani na Iran kuhusu vita inayoendelea eneo la Mashariki ya Kati, pamoja na kuruhusu meli za mafuta kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz. Hatua hizo zimechangia kupunguza ugumu katika usafirishaji na upatikanaji wa mafuta duniani.
Hata hivyo, wastani wa bei katika soko la dunia bado haujarejea katika kiwango kilichokuwepo kabla ya kuanza kwa vita hiyo tarehe 28 Februari 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment