NA: MWANDISHI WETU, DODOMAUwasilishwaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/27, uliofanywa na Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Omar, Juni 11, 2026, Bungeni, Jijini Dodoma, umetoa mwelekeo wa nchi katika juhudi za maendeleo na kutatua kero za wananchi katika sekta mbalimbali.Katika bajeti hiyo, serikali inatarajia kukusanya na kutumia shilingi trilioni 62.33 ambapo ni ongezeko la asilimia 10.3, ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2025/2026.Akizungumzia bajeti hiyo, Juni 12, 2026, Jijini Dodoma, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Umoja na Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda amesema ni dhahiri Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kwa vitendo kuwa ni mjenga nchi.Chatanda amesema bajeti hiyo inaakisi mahitaji ya wananchi katika kuwaletea maendeleo na imegusa sekta muhimu za kijamii na kiuchumi."Bajeti hii ni ya namna yake, mikopo ya vijana, wanawake na wenye mahitaji maalum imeongezeka kutoka asilimia kumi hadi 15. Pia, fedha nyingi zimetengwa kugharamia ujenzi wa bandari, barabara, viwanja vya ndege, reli ya kisasa ya SGR na reli ya TAZARA," amesema Chatanda.Aidha, Chatanda ameipongeza serikali kwa kuja na mikakati ya kulinda viwanda vya ndani na malighafi zake, sambamba na kuwakumbuka watengeneza maudhui mtandaoni kwa kuboresha mazingira ya kazi zao."Hata hili la serikali kutoa msamaha wa kodi na ushuru kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, hii ni hatua kubwa katika kuinua viwanda vyetu. Vilevile, vijana wetu wa sekta ya sanaa hasa wanaotengeneza maudhui ya mtandaoni nao wamekumbukwa kwa kupunguziwa tozo kwa asilimia 90," amesisitiza.Kadhalika, Chatanda amepongeza mwamko wa wananchi kulipa kodi kwa hiari, jambo lililowezesha bajeti hiyo kubebwa na Watanzania wenyewe kwa asilimia kubwa."Ukiangalia bajeti hii, kwa asilimia 74.2 ni mapato ya ndani, hili kamwe haliwezi kutenganishwa na mwamko wa wananchi kulipa kodi kwa hiari na kufanyiwa kazi maelekezo ya Rais Dk. Samia kwa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) kuhusu kutanua wigo wa wawalipa kodi, kusikiliza na kutatua kero zao," amesema.Bajeti hii inategemewa kuwa msaada mkubwa katika juhudi za ujenzi wa Taifa kutokana na kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kukuza kilimo, uvuvi, madini, ajira, michezo, utalii, nishati safi, uchumi wa kidijitali na bima ya afya kwa wote. Rais Dk. Samia na wasaidizi wake wa Ikulu ni miongoni mwa Watanzania waliofuatilia mbashara uwasilishwaji wa bajeti hiyo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment