" HATUA YA TANROADS YAIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WAKAZI WA BIMA NA CUOM JIJINI MBEYA

HATUA YA TANROADS YAIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WAKAZI WA BIMA NA CUOM JIJINI MBEYA

Na Lydia Lugakila Misalaba MediaMBEYAKwa miaka kadhaa, wananchi wa maeneo ya Bima na karibu na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mbeya (CUoM) wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na ongezeko la ajali za barabarani zilizokuwa zikihatarisha maisha ya watembea kwa miguu na wanafunzi.Baadhi ya ajali hizo zilisababisha vifo na majeruhi, hali iliyowalazimu wananchi kuendelea kuomba hatua za haraka za kuboresha usalama katika eneo hilo.Kufuatia kilio hicho, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya umechukua hatua ya kufunga taa za kuongoza magari ili kudhibiti ajali na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara.Wakazi wa maeneo hayo wanatarajia kuondokana na changamoto ya ajali za mara kwa mara kufuatia uwekaji wa taa hizo, ambao unatajwa kuwa sehemu ya juhudi za kuboresha usalama wa barabarani katika eneo hilo.Baadhi ya wakazi wameeleza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakishuhudia ajali mbalimbali zinazohusisha watembea kwa miguu na wanafunzi, hali iliyosababisha kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa watu kadhaa.Akizungumza kuhusu hali hiyo, Ernest Kashinje amesema eneo la Bima limekuwa miongoni mwa maeneo yenye matukio mengi ya ajali jijini Mbeya.Amebainisha kuwa moja ya ajali za hivi karibuni ilihusisha mwanafunzi aliyepoteza maisha baada ya kugongwa na gari, jambo lililoibua huzuni na wasiwasi mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo.Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Suleiman Bishanga, amesema uamuzi wa kufunga taa hizo umetokana na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi kuhusu ongezeko la ajali katika eneo hilo.Amesema uwekaji wa taa hizo unalenga kuongeza usalama kwa watumiaji wa barabara, hususan wanafunzi na watembea kwa miguu, pamoja na kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.Hatua hiyo imepokelewa kwa matumaini makubwa na wakazi wa maeneo ya Bima na CUoM, ambao wanaamini kuwa itasaidia kuokoa maisha ya watu wengi na kuifanya barabara hiyo kuwa salama zaidi kwa watumiaji wote.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post