" Mkutano wa Nishati Safi Watoa Dira ya Matumizi ya Asilimia 80 ifikapo 2034

Mkutano wa Nishati Safi Watoa Dira ya Matumizi ya Asilimia 80 ifikapo 2034

Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha Mkutano wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2026 umekuwa jukwaa muhimu  lililowakutanisha viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo, wawekezaji na wananchi kujadili njia bora za matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa hilo Jijini Arusha Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba amesema Lengo la jukwaa hilo ni  kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa ambao unaathiri mazingira na afya za watu.Aidha amesema mkutano huo pia unalenga kutoa elimu kuhusu faida za matumizi ya gesi, majiko banifu na teknolojia nyingine za kisasa za kupikia." Kupitia mijadala na maonesho mbalimbali, wananchi wanapata nafasi ya kuelewa umuhimu wa nishati safi katika kuboresha maisha ya familia na kulinda mazingira kwa vizazi vijavyo na  kutoa fursa kwa wawekezaji na kampuni mbalimbali kuonesha bidhaa na huduma zinazohusiana na nishati safi ya kupikia.Hata hivyo Makamba amesema kuwa hatua hiyo imesaidia kukuza biashara, kuongeza ajira na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika kuhakikisha wananchi wengi wanapata huduma za nishati safi kwa gharama nafuu.Kwa ujumla, Mkutano wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2026 unatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya nishati nchini,mkutano huo, Tanzania itaendelea kuchukua hatua muhimu katika kulinda mazingira.Kwa upande wake Mkurugenzi wa nishati safi ya kupikia Nolasco Mlay amesema safari ya matumizi ya nishati safi nchini ilianza mwaka 2021 ambapo kiwango cha matumizi kilikuwa asilimia 6 pekee. Katika kipindi cha miaka mitano, juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali pamoja na wadau wa maendeleo zimewezesha kiwango hicho kufikia asilimia 28, hatua inayodhihirisha mafanikio makubwa katika sekta ya nishati safi.Vile vile amesema ongezeko hilo limechangiwa na kampeni za uhamasishaji kwa wananchi, upatikanaji wa teknolojia za kupikia kwa kutumia nishati safi pamoja na ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za serikali. Mlay amesema hatua hizo zimeendelea kusaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira na athari za kiafya kwa wananchi."Licha ya mafanikio hayo, bado kuna haja ya kuongeza jitihada kutoka kwa kila mmoja pamoja na serikali ili kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanaendelea kuongezeka, lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 kiwango cha matumizi ya nishati safi kinafikia asilimia 80, hatua itakayosaidia kulinda mazingira, kuboresha afya za wananchi na kukuza maendeleo endelevu nchini" amesema Mlay.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post