" CHATANDA: SINGAPORE IMEJIRIDHISHA NA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI YALIYOPO TANZANIA

CHATANDA: SINGAPORE IMEJIRIDHISHA NA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI YALIYOPO TANZANIA

NA: MWANDISHI WETU, DODOMATanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara ambayo yanawavutia viongozi, wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuwekeza na kuchangia ukuaji wa maendeleo na uchumi.Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Mary Chatanda Juni 10, 2026, Jijini Dodoma, kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Singapore, Tharman Shanmugaratnam nchini."Ujio wa Rais wa Singapopre nchini ni kielekezo cha kuimarika kwa diplomasia nchini. Lakini tukumbuke pia ujio wake ni wa kimkakati, kuhakikisha Singapore na Tanzania zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ya kimaendeleo. Wenzetu wa Singapore wamejiridhisha pasi na shaka juu ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo Tanzania,"amesema Chatanda.Sanjari na hilo, Chatanda amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya maboresho makubwa ya mazingira ya uwekezaji na biashara ambapo wawekezaji wameongezeka."Kila mwenye macho anajionea namna Rais wetu Dk. Samia alivyoboresha mazingira ya uwekezaji. Mazingira ya biashara yamekuwa rafiki kwa yeyote mwenye dhamira ya kweli ya kuwekeza nchini, ndiyo maana kumekuwa na kasi kubwa ya wawekezaji kuja nchini," amesisitiza Chatanda. Katika hatua nyingine, Chatanda amewahimiza Watanzania na wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na uwekezaji kwani dhamira ya serikali ni kuhakikisha wananachi wazawa wananufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo na ya kimkakati. "Wanawake wenzangu tusilale, Rais wetu ameshafungua milango ya fursa ya biashara na uwekezaji, tutumie fursa hii kwani wanawake ni wadau muhimu katika juhudi za maendeleo," amesema Chatanda.Juni 9, 2026, Rais Dk. Samia na Rais Shanmugaratnam walishiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Tanzania na Singapore, lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.Katika Kongamano hilo, Rais Dk. Samia alitaja maeneo muhimu ya ushirikiano na Singapore ili kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo. Maeneo hayo ni pamoja na bandari na usafirishaji, uongezaji thamani katika madini na kilimo. Pia, nishati jadidifu na miundombinu ya kisasa. Eneo jingine ni utalii, ukarimu na uchumi wa buluu pamoja na huduma za kifedha na utatuzi wa migogoro ya kibiashara.Aidha, makubaliano hayo pia yamehusisha kuondoka kodi mara mbili na kuzuia ukwepaji wa kodi, maendeleo na uendelezaji wa ujuzi, biashara ya kaboni na uwezeshaji wa biashara. Vilevile, maendeleo ya vijana na uchumi wa kidijitali."Uwezo wetu ni mkubwa zaidi ya kiwango cha biashara na uwekezaji tulichofikia sasa. Tumekubaliana kuongeza biashara na uwekezaji," amesema Rais Dk. Samia.Ikumbukwe kuwa Rais Dk. Samia amedhamiria kuimarisha diplomasia ya uchumi kwa kuhakikisha Tanzania inajenga mahusiano mazuri na mataifa mengine ikiwa ni njia ya kuchochea maendeleo kupitia biashara na uwekezaji kwa maendeleo endelevu. Tayari mahusiano ya Tanzania na Singapore yametimiza miaka 45 tangu yalipoasisiwa mwaka 1980.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post