" RAIS SAMIA ANAYAJALI MAKUNDI MAALUM, AMEONGEZA MIKOPO KUTOKA ASILIMIA 10 HADI 15 - CHATANDA

RAIS SAMIA ANAYAJALI MAKUNDI MAALUM, AMEONGEZA MIKOPO KUTOKA ASILIMIA 10 HADI 15 - CHATANDA

NA: MWANDISHI WETU, DODOMA

Wanawake, vijana na wenye mahitaji maalum sasa wamefikiwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, kufuatia bajeti hiyo kuongeza asilimia za mikopo ya makundi hayo kutoka asilimia kumi hadi 15.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mary Chatanda, Juni 23, 2026, Jijini Dodoma, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anayajali makundi hayo kwa maneno na kwa matendo, ndiyo maana ameamua kuongeza asilimia za mikopo yao.

"Uwezeshaji wananchi kiuchumi hasa makundi ya wanawake, vijana na wenye mahitaji maalum ni miongoni mwa vipaumbele vya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameona asilimia kumi haitoshi, ameongeza asilimia tano zaidi ili kuhakikisha makundi hayo yananufaika na fursa za kiuchumi kwa ustawi wao," amesema Chatanda.

Sambamba na hilo, Chatanda amesema katika mipango ya maendeleo ni vyema kuhakikisha makundi yote yanajumuishwa ili maendeleo tarajiwa yaweze kugusa watu wote kwani hayo ndiyo maendeleo lenye tija kwa Taifa.

"Tanzania tunajenga uchumi shindani na jumuishi, kwa kuhakikisha hilo linafikiwa, ndiyo maana makundi haya yanapewa kipaumbele kwani mafanikio yao yana mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa zima," amesema.

Kadhalika, Chatanda amesisitiza makundi hayo wapewe mafunzo ya kutosha ya kiujasiriamali ili waweze kutumia vyema mikopo hiyo katika kujiletea maendeleo.

"Maofisa wetu wa maendeleo ya jamii ngazi za kata na wilaya kwa kushirikiana na taasisi za fedha kama mabenki, watoe mafunzo ya namna bora ya kufanya biashara na shughuli nyingine za kiuchumi, ili waweze kuwa na uwezo wa kurejesha mikopo hiyo," amesisitiza.

Katika mabadiliko chanya yaliyofanyika katika bajeti ya mwaka 2026/2027, ni kuongeza asilimia za mikopo kutoka kumi hadi 15 ili kuwezesha makundi hayo kunufaika zaidi kiuchumi likiwepo suala la uboreshaji wa mazingira ya kufanyia shughuli zao za kiuchumi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post