

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo ya kina na Mwenyekiti pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dangote Group, Alhaj Aliko Dangote, katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Dangote ambaye ni mfanyabiashara na mwekezaji kinara barani Afrika, ameeleza utayari mkubwa wa kampuni yake katika kupanua wigo wa ushirikiano wa uwekezaji na Serikali ya Tanzania kupitia sekta mbalimbali za kimkakati nchini.
Maeneo makuu yaliyoguswa kwenye mazungumzo yao yanajumuisha miundombinu ya usafirishaji, uzalishaji wa mbolea hapa nchini, pamoja na sekta ya nishati, ambayo yote kwa pamoja yanaonekana kuwa fursa muhimu zinazoweza kuchochea na kuamsha shughuli za kiuchumi sio tu ndani ya Tanzania bali pia katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Dangote amebainisha kuwa Tanzania ina mazingira mazuri sana ya uwekezaji na fursa kubwa za kukuza viwanda vinavyoongeza thamani ya malighafi pamoja na kuchochea biashara za kikanda, huku akisisitiza kuwa wametambua maeneo yenye manufaa makubwa na wako tayari kushirikiana na Serikali kuyaendeleza kwa faida ya pande zote mbili.
Kwa upande wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepokea kwa mikono miwili nia hiyo na tayari amezielekeza wizara na taasisi husika kuendelea na majadiliano ya kitaalamu kuhusu maeneo yaliyojadiliwa, kwa kuzingatia sera, sheria, na vipaumbele vya maendeleo ya nchi.
Rais amehitimisha kwa kueleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi ili kuvutia uwekezaji wenye tija unaochochea ukuaji wa uchumi, maendeleo ya viwanda, uhamishaji wa teknolojia, na utengenezaji wa ajira kwa Watanzania.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment