" SANGU FC YATINGA HATUA YA TIMU 12 BORA BAADA YA KUIONDOA BULIGE FC NIACHEKONA CUP 2026

SANGU FC YATINGA HATUA YA TIMU 12 BORA BAADA YA KUIONDOA BULIGE FC NIACHEKONA CUP 2026

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mabingwa watetezi wa mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Sangu FC kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, wamefanikiwa kutinga hatua ya timu 12 bora baada ya kuiondoa Bulige FC kutoka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kwa faida ya mabao ya jumla katika michezo miwili.

Katika mchezo wa marudiano uliochezwa leo Jumamosi Juni 6, 2026  katika Uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa Mkoani Shinyanga, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 katika pambano lililokuwa na ushindani mkubwa kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho.

Matokeo hayo yanaifanya Sangu FC kuendelea na mashindano hayo kutokana na faida waliyoipata katika mchezo wa kwanza ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bulige FC.

Kwa kujumlisha matokeo ya michezo yote miwili, Sangu FC imefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 (aggregate) na hivyo kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya timu 12 bora huku safari ya Bulige FC katika mashindano hayo ikifikia tamati.

Kwa upande wao, viongozi wa Bulige FC wamemshukuru mwandaaji wa mashindano hayo kwa kuwapa nafasi ya kushiriki huku wakiahidi kurejea kwa nguvu zaidi katika mashindano yajayo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano, Sambayi Jilya, amesema kuanzia kesho Jumapili mashindano yataingia rasmi katika hatua ya timu 12 bora ambapo michezo itachezwa kwa mfumo wa mtoano wa moja kwa moja, timu itakayofungwa ikiondolewa mara moja kwenye mashindano hayo.

Baadhi ya michezo iliyopangwa kuchezwa katika hatua ya timu 12 bora ni pamoja na:

Nyundo FC dhidi ya Mawemiru FC, Duara FC dhidi ya Songambele Mhangu FC na Home Boys FC dhidi ya Ufukunyungu FC

Ameendelea kuwakaribisha wananchi, wadau wa michezo na mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwabenda kushuhudia michezo ya hatua hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na mdau wa michezo Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa shirika la Lushu Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha amani na kukuza michezo katika jamii.

Kwa mawasiliano ya Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757 267 738.

NIACHEKONA CUP MWABENDA – WEKA TU WEKE.

Kikosi cha Bulige FC na kocha wa timu.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post