" SENEGAL YAFUFUA MATUMAINI YA KUTINGA HATUA YA 32 BORA KOMBE LA DUNIA 2026

SENEGAL YAFUFUA MATUMAINI YA KUTINGA HATUA YA 32 BORA KOMBE LA DUNIA 2026

 

Timu ya Taifa ya Senegal imefufua matumaini ya kutinga hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Iraq mabao 5-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi I uliochezwa kwenye Uwanja wa Boston, Jimbo la Massachusetts, Marekani.

Licha ya ushindi huo mnono, Senegal italazimika kusubiri matokeo ya makundi mengine ili kujua kama itafuzu hatua ya mtoano kama moja ya timu bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu.

Senegal ilianza mchezo kwa kasi na kufungua ukurasa wa mabao dakika ya nne kupitia Habib Diarra, aliyemalizia mpira wa kona uliopigwa na Lamine Camara baada ya shambulizi lililoanzishwa na Abdoulaye Seck.

Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa Iraq dakika ya 13, baada ya nahodha wao Rebin Sulaka kumuangusha Sadio Mane akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga. Mwamuzi Anthony Taylor hakusita kutoa kadi nyekundu ya moja kwa moja, na kuiacha Iraq ikicheza na wachezaji 10 kwa zaidi ya dakika 80.

Hata hivyo, kipa Ahmed Basil aliokoa mkwaju wa faulo wa Mane na kuifanya Iraq kuendelea kuwa na matumaini licha ya kucheza pungufu.

Kipindi cha pili kilitawaliwa na Senegal. Ismaila Sarr alifunga bao la pili dakika ya 56 akimalizia pasi ya Lamine Camara, kabla ya Pape Gueye kuongeza la tatu dakika ya 59 muda mfupi baada ya kuingia akitokea benchi.

Gueye aliendelea kung’ara kwa kufunga bao lake la pili na la nne kwa Senegal dakika ya 71 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Iliman Ndiaye. Dakika ya 82, Ndiaye naye alijiunga kwenye orodha ya wafungaji kwa shuti lililomshinda kipa Jalal Hassan, aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ahmed Basil, na kuhitimisha ushindi wa mabao 5-0.

Pape Gueye alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi baada ya kufunga mabao mawili na kuchangia kwa kiwango kikubwa ushindi huo.

Ushindi huo umeingia kwenye historia ya soka la Afrika kwa kuwa ndio ushindi mkubwa zaidi kuwahi kupatikana na timu ya Afrika katika fainali za Kombe la Dunia.

Senegal, iliyomaliza hatua ya makundi ikiwa na pointi tatu, sasa inasubiri matokeo ya makundi mengine ili kuona kama itafuzu kupitia nafasi ya timu bora nane zilizomaliza katika nafasi ya tatu.

Kwa upande wa Iraq, ilikuwa ni mwisho mbaya wa kampeni yao ya pili katika historia ya Kombe la Dunia. Kikosi hicho kinachonolewa na Graham Arnold kilimaliza hatua ya makundi bila pointi hata moja, kikiendeleza rekodi ya kutoshinda wala kutoka sare katika mechi zote sita ilizowahi kucheza kwenye fainali za Kombe la Dunia.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post