" SERIKALI YAWEKA WAZI MIKAKATI YA MIKOPO NAFUU KWA VIJANA NA MAKUNDI MAALUMU BUNGENI

SERIKALI YAWEKA WAZI MIKAKATI YA MIKOPO NAFUU KWA VIJANA NA MAKUNDI MAALUMU BUNGENI

 

Serikali imesisitiza kuwa inaendelea kutekeleza mpango wa muda mrefu wa kuwawezesha vijana nchini, wakiwemo wenye mahitaji maalumu, kupitia vikundi vilivyosajiliwa ili kuimarisha ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa.

 Hatua hiyo inalenga kuhakikisha vijana wanapata fursa sawa za kujikwamua kiuchumi kupitia mifumo rasmi iliyowekwa na serikali.

Uwezeshaji huo unahusisha utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kupitia vyanzo vikuu vitatu ambavyo ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Programu ya Uwezeshaji Vijana Kiuchumi inayotekelezwa kupitia Shilingi bilioni 200 za ahadi ya rais, pamoja na mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kote nchini.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana.

 Mwinjuma alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Latifa Juwakali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kuwasaidia vijana wenye vikundi vilivyosajiliwa na wenye mahitaji maalumu.

Mbali na mikopo hiyo, Naibu Waziri alibainisha kuwa serikali inaendelea kutekeleza utaratibu wa kutenga asilimia 30 ya zabuni za umma kwa makundi maalumu, kuunganisha vikundi vya vijana na taasisi za kifedha, pamoja na kuimarisha mifumo ya uratibu na taarifa.

 Hatua hizi zote zinalenga kuongeza fursa za ajira, ujasiriamali, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa vijana nchini.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post