
Staa wa filamu nchini, Wema Sepetu, amefanikiwa kupata mtoto wa kiume baada ya kujifungua jana, jambo lililopokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki, marafiki pamoja na mastaa mbalimbali.
Siku chache kabla ya kujifungua, Wema aliandaa hafla maalum ya baby shower iliyohudhuriwa na mastaa kadhaa wa tasnia ya burudani, marafiki na ndugu wa karibu. Hafla hiyo ilitawaliwa na nyuso za furaha, dua na pongezi kwa mama mtarajiwa, huku wageni wakimtakia kila la heri katika safari yake ya uzazi.
Ujio wa mtoto huyo umehitimisha safari ndefu ya Wema ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mama, jambo ambalo limegusa wengi ndani na nje ya tasnia ya burudani.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment