" Mastaa Wampongeza Wema Sepetu Baada ya Kupata Mtoto wa Kiume

Mastaa Wampongeza Wema Sepetu Baada ya Kupata Mtoto wa Kiume

Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu akiwa na mpenzi wake, Whozu.

Mastaa mbalimbali wamefurika kwenye ukurasa wa Instagram wa msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, kumpongeza baada ya kuthibitisha kuwa amejifungua mtoto wa kiume.

Wema Sepetu, amejifungua mtoto wa kiume Juni 12, 2026 majira ya saa 11 jioni katika Hospitali Saifee jijini Dar es Salaam.

Habari za kujifungua kwake zilianza kusambaa usiku wa kuamkia leo Juni 13 kabla ya Wema mwenyewe kuthibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa ujumbe ulioonyesha furaha yake kubwa baada ya kupata mtoto, mashabiki na watu mbalimbali wakimpongeza yeye pamoja na mpenzi wake, Whozu, kwa hatua hiyo muhimu katika maisha yao.

Furaha hiyo imegusa wengi kutokana na safari ndefu aliyopitia Wema katika ndoto yake ya kuwa mama. Kwa miaka kadhaa, Wema amekuwa akizungumza hadharani kuhusu hamu yake ya kupata mtoto na changamoto mbalimbali alizokutana nazo katika safari hiyo. Mara kadhaa aliweka wazi maumivu aliyoyapata baada ya kupoteza ujauzito, jambo lililowagusa mashabiki wake na kuifanya habari ya kujifungua kwake kupokelewa kwa hisia kubwa.

Baada ya Wema kuweka ujumbe uliodokeza ujio wa mtoto wake, mastaa kadhaa walitumia sehemu ya maoni kutoa pongezi zao.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez, aliandika: “Hongera sana mpendwa wangu! Karibu duniani mtoto wa kiume 🥹💙 Mungu ni mwema wakati wote!”

Kwa upande wake, Zamaradi Mketema aliandika kwa hisia:

“Oooooh!!! 😢❤️❤️

Naye sosholaiti maarufu Kayitesi Abdul Tessy alitoa pongezi zake kwa kuandika:

“Nyinyiiii 😍… Maashallah ❤️

Pongezi zimeendelea kumiminika kutoka kwa mashabiki, marafiki na watu maarufu mbalimbali wakimtakia Wema na mwanawe afya njema na maisha yenye furaha.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post