" Whozu Avunja Ukimya Baada ya Wema Sepetu Kujifungua Mtoto wa Kiume

Whozu Avunja Ukimya Baada ya Wema Sepetu Kujifungua Mtoto wa Kiume

 

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Whozu, ameonyesha hisia zake za furaha baada ya mpenzi wake, Wema Sepetu, kujifungua mtoto wa kiume.

Kupitia ujumbe wake, Whozu amesema ujio wa mtoto wao ni uthibitisho kuwa uwezo wa Mungu ni mkuu kuliko matarajio na makadirio ya binadamu.

“Sio kuwa tu wazuri sana mbele zake lakini ilimpendeza aonyeshe ukuu wake kwenye uso wa dunia kuwa makadirio ya wanadamu hayawezi kushinda kudra zake…”

Whozu aliendelea kueleza kuwa tukio hilo ni kibali maalum kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya kipindi kirefu cha maombi na subira.

“Hakika Mwenyezi Mungu amejidhihirisha na kutupa kibali🙏🏼.”

Katika ujumbe huo, msanii huyo alimpongeza Wema huku akitoa shukrani kwa wote waliokuwa wakiwasapoti na kuwaombea.

“Hongeraa shunu wangu na akhsanteni nyote mliokuwa mkituombea. Mungu yupo na wanaomtumaini. Tusichoke kukesha tukiomba maana yeye ni mwenye huruma siku zote🙏🏼.”

Ujumbe huo umeibua hisia kubwa kwa mashabiki wengi, hasa kutokana na safari ndefu ya Wema ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mama, huku wengi wakitafsiri tukio hilo kama ushindi wa imani, subira na matumaini.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post