" THBUB YAWAFIKIA ZAIDI YA WANANCHI 89,000 KUPITIA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU

THBUB YAWAFIKIA ZAIDI YA WANANCHI 89,000 KUPITIA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU


Dar es Salaam

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendelea kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa kuwafikia zaidi ya wananchi 89,000 kupitia njia mbalimbali za utoaji elimu katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Tume hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Mawasiliano,Utafiti na Nyaraka wakati akiongea na vyombo vya habari katika viwanja vya  Maonesho ya Kimataifa ya Biashara saba saba leo Juni 29,2029

Akielezea kuhusu njia zilizotumika kufikisha elimu hiyo , Bi. Mnanka amesema  njia hizo ni mafunzo kwa makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo Askari wa jeshi la Polisi , waandishi wa habari na madiwani, vipindi vya redio na televisheni, mitandao ya kijamii, huduma ya ujumbe mfupi wa simu (Bulk SMS) pamoja na usambazaji wa vipeperushi na machapisho ya elimu.

Aidha, Bi. Mnanka amesema katika kipindi hicho, wananchi zaidi ya 80,000 walifikishiwa ujumbe wa elimu kupitia simu za mkononi, huku vipeperushi 39,129 na vitabu 200 vya elimu vikisambazwa kwa wananchi ili kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu, utawala bora na namna ya kuwasilisha malalamiko THBUB.

Vile vile , Tume ilirusha vipindi 79 vya elimu kupitia redio na televisheni, hatua iliyochangia kuwafikia wananchi wengi zaidi nchini.

Bi. Mnanka amesema kiwa THBUB itaendelea kutumia teknolojia, majukwaa mbalimbali na kushirikiana na wadau majukwaa kuhakikisha elimu ya haki za binadamu inawafikia Watanzania wengi zaidi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post